TIGO YADHAMINI UZINDUZI WA ROCK CITY MALL: KUFANYA GULIO LA KUUZA BIDHAA MBALIMBALI MWANZA

Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Mwanza hivi karibuni, ambapo jengo la kimataifa la biashara (Rock City Mall) limekamilika na Tigo watafanya gulio la kuuza bidhaa mbalimbali. Kushoto ni Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa Mwanza City Commercial Complex Company Limited, Joseph Mlinzi na kulia ni Meneja wa Tigo Pesa Kanda ya Ziwa Issa Orry.
Meneja wa Tigo pesa Kanda ya Ziwa Issa Orry, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hivi karibuni, ndani ya jengo la kimataifa la biashara (Rock City Mall) ambapo limekamilika na Tigo watafanya gulio la kuuza bidhaa mbalimbali. Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo.
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mwanza City Commercial Complex Company Limited, Joseph Mlinzi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hivi karibuni, kuhusu kukamilika kwa jengo la kimataifa 
la biashara (Rock City Mall), ambalo wananchi wanaruhusiwa kuingia na kununua bidhaa kuanzia jumamosi wiki hii. Kulia ni Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo, ambapo Tigo wataendesha gulio la kuuza bidhaa zao.