WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA TAWI JIPYA LA BENKI YA POSTA MJINI SONGEA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, (wa pili kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu, na Watu Wenye Ulemavu), Bi. Jenista Mhagama, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, (wa kwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa tawi jipya la benki hiyo mjini Songea juzi Januari 4, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kadi ya akaunti yake ya Benki ya Posta Tanzania aliyokabidhiwa baada ya kuifungua alipokuwa akifungua tawi la Benki hiyo la Songea Januari 4, 2016.
Waziri Mkuu akiagana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, baada ya kufungua tawi la benki hiyo mjini Songea Januari 4, 2016. Wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa benki hiyo Bi. Mystica Mapunda Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani yenye nembo ya TPB, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya Waziri Mkuu kufungua tawi jipya la benki hiyo mjini Songea juzi Januari 4, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu.
Tawi jipya la TPB linavyoonekana.