Dar es Salaam, 11 December 2015 – Kampuni ya ndege ya gharama nafuu barani Afrika, fastjet imetangaza safari zake za kila siku kwenda Zanzibar kutoka Dar es Salaam zitakazoanza tarehe 16, Januari 2016.
Huduma hii ambayo itaanza mara moja ni matokeo ya maombi ya abiria na makampuni yanayotoa huduma kwa watalii ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakidai huduma hiyo ili kuimarisha soko la ndani.
Huduma za usafiri kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere wa Dar es Salaam na ule wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar zitafanywa kwa kutumia aina ya ndege ya Airbus A319 yenye uwezo wa kubeba abiria 165.
Uanzishwaji wa safari hizo ambazo zitakuwa pia zinapitia Johannesburg, Afrika ya Kusini ni katika kutekeleza sera ya fastjet ya kusikiliza madai ya wateja wake.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania Jimmy Kibati, safari ya kutoka Zanzibar zitaanza saa 3:30 asubuhi na kuwasili saa 7:20, na baadae kutua Zanzibar saa 1:40 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Safari hizi mpya zitakuwa ni faraja kwa wale abiria wa ndani na nje ambao wanasafiri kwa madhumuni ya kupumzika ili kukamilisha shughuli zao muhimu kibiashara kwani sasa watapata nafasi ya kuchagua siku za kusafiri ili kukamilisha malengo yao, na sivyo kama ilivyokuwa hapo awali ambapo iliwalazimu kusafiri kati ya siku za Junanne au Alhamisi.
Tiketi kwa safari ya kwenda Zanzibar sasa zinauzwa kwa safari ya kwenda tu kutoka Dar es Salaam kuanzia shilingi elfu 22,000 na nauli ya kutoka Zanzibar kuanzia shilingi elfu 22,000, na kufanya nauli ya kwenda na kurudi Zanzibar kutoka Dar es Salaam kuanza na shilingi elfu 70,000 hii ikiwa ni pamoja na gharama za malipo ya uwanja pamoja na kodi ya serikali.
Aidha, nauli ya safari moja tuu ya kutoka Johannesburg kwenda Zanzibar itaanza na Randi ZAR 1,704, na ile ya safari moja kutoka Zanzibar itaanza na Randi ZAR 1,860, ilhali safari ya kwenda na kurudi kisiwani Zanzibar kutoka Johannesburg itaanza na randi ZAR 3,564 na hii ni pamoja na gharama za uwanja na kodi ya serikali.
Gharama ndogo za fastjet zitakazotozwa kuanzia Dar es Salaam kwenda Zanzibar zitakuwa rahisi sana kuliko zile gharama zinazotozwa na ndege zingine zinazofanya safari zao kupitia safari hii ambazo kwa kawaida hufanya safari zao mara mbili kwa wiki.
Itakuwa ni faraja kubwa kwa wasafiri wa kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambao watakuwa wanalipa nauli ya shilingi elfu 70,000 tuu kwenda na kurudi wakati wa mwezi huu wa Disemba na kuendelea na Januari na Februari 2016.
Kwa sasa, abiria wa fastjet wanaenda Zanzibar kwa ndege za kampuni ya Coastal Aviation kutokana na makubaliano ya kampuzi hizo mbili, lakini safari hizo za angani zilipewa masharti ya kusafirisha abiria wao wakati wa mchana na vilevile abiria wanalazimika kupokea mizigo yao kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
“Abiria wa Fastjet wanaohitaji kusafiri kwenda Zanzibar watafanya chaguo la kuamua siku za kuondoka na hakuna ambao watalazimika kuanza safari zao ama kati ya Jumanne au Alhamisi, ilimradi tu maamuzi yao yatategemea mahitaji ya abiria mwenyewe”, alisema Kibati.
“Kinachozingatiwa hapa ni kwamba, kulipa nauli kidogo maana yake ni kwamba wale ambao watapenda kusafiri siku za mapumziko sasa watakuwa wanafanya maamuzi ya kutayarisha malazi ama kusafiri pamoja na familia zao badala ya kuwaacha watoto wao nyumbani wakiwa na babu zao ama walezi wao”, Kibati aliongeza.
Kwa kutumia garama nafuu za nauli za ndege ya fastjet ambazo zinakaribia nusu ya gharama kamili ya nauli zinazotumika kwa hivi sasa, fastjet inategemea kuwapata abiria wengi ambao watajitokeza kusafiri kwa mara yao ya kwanza kwenda Zanzibar, na ambao bila ya unafuu huu wasingeweza kugharamia nauli zilizokuwepo hapo awali za kusafiri kwenda Zanziba.
Matumaini haya yanaungwa mkono na utafiti uliofanywa hivi karibuni na kampuni ya fastjet ambapo matokeo ya utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 35 ya abiria wake ilikuwa ndiyo mara yao ya kwanza ya kusafiri kwa ndege na waliweza kumudu gharama za safari.
“Nauli rahisi huwafanya watalii pamoja na wageni wengine kusafiri kwenda Zanzibar ambapo hurahisisha na kupanua utalii wa ndani kisiwani Zanzibar na ambayo pia huchangia katika kukua kwa uchumi kisiwani humo”, anasema Kibati.
· Safari za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar zitaanza tarehe 11/1/2016.
· Ndege itaanza safari zake kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam mara moja kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa mara mbili katika siku za Jumanne, Jumatano, Alhamisi na siku wa mwisho wa wiki kuanzia tarehe 11, Januari 2016 mpaka tarehe 21, Machi 2016.
Kuhusu Fastjet Tanzania:
Fastjet Tanzania, ni ndege itoayo huduma ya bei nafuu ambayo ilianza kazi hapa Tanzania Novemba 2012. Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ubora na usalama, shirika la ndege la fastjest imeanzisha mtindo mpya wa usafiri wa anga barani Afrika kwa kutoza nauli nafuu zinazoweza kugaramiwa na abiria yeyote yule kwa kutumia ndege yake ya aina ya Airbus A319s. Fastjet imeweza kuharakisha huduma nafuu kwa abiria wake nchini Tanzania na seheme zingine barani Afrika kwa ujumla.
Matokeo ya huduma zao kwa wateja zinaonyesha kuwa imefikia asilimia 100 kwa utoaji wa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa. Na katika kuendeleza huduma zake hapa nchini, kampuni ya Fastjet imekuwa ikishinda tuzo mbalimbali zikiwemo zile "Brand Strategy of the Year" na ile ya 2014’s Drum Marketing Awards in London, pamoja na ile tuzo ya mbunifu wa usafiri yaani, “the Transport Innovator” iliyotolewa jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini
Kwa maelezo zaidi kwa umma kuhusu kampuni Wasiliana na:-
Lucy Mbogoro-Public Relations and Marketing Executive, Fastjet Tanzania
+255-22 2866130/3/4/6 +255-713-843975
Lucy.mbogoro@Fastjet.com