BENKI YA NBC YATOA SOMO KUHUSU UBORA WA HUDUMA YAKE YA ISLAMIC BANKING KWA WATEJA WA MTWARA

Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo kuhusu huduma za kibenki zinazofuata kanuni na misingi ya kiislamu (Islamic Banking) katika warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC mkoani Mtwara hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu (Islamic Banking), cha Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia), akielezea kuhusu huduma hizo wakati wa warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC mkoani Mtwara hivi karibuni.
Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kulia), akiagana na mmoja wa wateja wao Mohamed Kioze mara baada ya kuisha warsha ya siku moja waliyowaandalia wateja wa NBC kwa ajili ya kuwaelezea kuhusu bidhaa mbalimbali zinazopatikana kupitia kitengo cha Islamic Banking cha NBC, mjini Mtwara hivi karibuni.